UFARANSA:MAOUNDOU AHITAJIWA NA JESHI LA POLISI NCHINI MALI.
Kufuatia ombi lilitolewa na Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta kwa kijana, Mamoudou Gassama ambaye amepata umaarufu baada ya kumuokoa mtoto aliyekuwa amening’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne katika jengo refu jijini Paris, Ufaransa watu mbalimbali wametoa maoni yao na kudai kuwa si jambo rahisi kwa kijana huyo aliyepewa umaarufu wa Spiderman kukubali kurudi nchini kwake.
Ambapo mapema jana Rais wa Mali alimtaka Mamoudou Gassama kurejea nchini Mali na kulitumikia jeshi la polisi nchini humo kwani tayari ameshamwandalia nafasi ya kazi katika jeshi la polisi la Mali.
https://i1.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2018/05/mamoudou-gassama-fast-facts-about-malian-spiderman-who-climbed-building-to-save-child-dangling-from-balcony.jpg?w=800
Taarifa hizo ziliwasilishwa na Balozi wa Mali nchini Ufaransa, Toumani Djimé Diallo mara baada ya kuzungumza na kijana huyo katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo na kumpa pongezi kutoka kwa rais wa Mali.
Aidha baadhi ya maoni mbalimbali ya watanzania wamesema Ombi la Rais wa Mali ni sawa na kumwambia msichana wa mjini achague pizza na mchicha wakimaanisha kuwa sio rahisi kwa kijana huyo kukubali kurudi nchini kwake Mali ilihali tayari ameshatambulika nchini ufaransa na kupewa uraia wa nchi hiyo ambao alikuwa akiutafuta kwa muda mrefu.
Hata hivyo mtandaoni tayari zimeanza kuzagaa baadhi ya picha za utani zikionesha watu mbalimbali wakikwaa maghorofa wakidai wanafanya uokoaji ili kupata zali alilopata Mamoudou Gassama.
Ukizingatia tayari Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika Jeshi la Zima moto la Ufaransa, pia amemtunukia medali ya kipekee ya ushujaa kijana huyo na kuwataka raia wote kuiga mfano wake.
0 on: "UFARANSA:MAOUNDOU AHITAJIWA NA JESHI LA POLISI NCHINI MALI. "