Game Reviews

PRESHA YA KUPANDA NA YA KUSHUKA

 


PRESHA YA  KUPANDA.
Hii hutokea pale nguvu ya msukumo wa damu inayosukumwa na moyo kwenda kwenye mishipa ya damu(Arteri) kuwa kubwa kuliko njia ya mishipa hiyo hivyo kushindwa kuhimili nguvu au mgandamizo huo wa damu,unaweza kuwa na tatizo hili la mgandamizo mkubwa wa damu(Hypertension) kwa mda mrefu bila kuhisi dalili zozote na kupelekea uharibifu wa mishipa ya damu kuzid kuendelea hadi kusababisha Shinikizo la damu(Heart Attack).

presha ya kupanda ni 140mmHg juu yaani pale mgandamizo wa damu unapozid wakati 90mmHg ni pale moyo unapojilegeza na kujaza damu kama visemavyo vipimo ya tatizo hii..Kwamba
~Presha ya kawaida(Normal) ni 120/80mmHg
~Presha ya kupanda(Hypertension)
Stage 1) 140/90mmHg
Stage 2) 160/100mmHg
Stage 3) 180/110mmHg
Presha kubwa zaidi(Hypertensive Crisis)     240/120mmHg.

SABABU ZA PRESHA YA KUPANDA

A) STAILI YA MAISHA
i) Kutojishughulisha/Uvivu.
ii) Chumvi nyingi kwenye chakula cha kusindikwa na chenye mafuta.
iii) Pombe na uvutaji wa Sigara.
iv) Chakula kisicho na madini ya Pottasium ya kutosha.

B) UMRI
i) Umri unapozidi kuwa mkubwa kuanzia miaka 60 kunauwezekano wa kupata tatizo hili.

C) JINSIA
-Wanaume wapo hatarini kupata kwenye umri mdogo wakati Wanawake hupatwa zaidi wanapokuwa na umri mkubwa.

D)KURITHI.

E)UZITO MKUBWA.

F)MSONGO WA MAWAZO.

DALILI ZA PRESHA YA KUPANDA

i) Kizunguzungu.
ii) Kichwa kuuma.
iii) Kutoona vizuri.
iv) Kichefuchefu.
v) Kubanwa na Pumzi.

MADHARA YA MGANDAMIZO MKUBWA WA DAMU.

i) Uvimbe mkubwa kwenye kuta za arteri(Aneurysm).
ii) kupanuka au kudhoofika kwa moyo hadi kufikia kishindwa kusukuma damu ya kutosha(Heart Failure).
iii) Kusinyaa kwa mishipa ya damu kwenye figo na moyo kusababisha vishindwe kufanya kazi,ubongo na miguu pia.
iv) kupasuka kwa mishipa ya damu na kusababisha macho kutoona Vizuri au Upofu kabisa.

*PRESHA YA KUSHUKA(HYPOTENSION)*
Hii hutokea pale mgandamizo wa damu usukumwao na moyo kupitia kwenye njia au kuta za mishipa ya damu(Arteri) kuwa mdogo kuliko upana wa mishipa yenyewe hivyo kupelekea damu chache kufika kwenye ubongo,figo na sehem nyingine za viungo mwilini.
Mfano wa Viwango Vyake ni:
     * 90/60mmHg.
     * 115/60mmHg.
     * 115/50mmHg.

DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA.

i)Kizunguzungu na kuanguka.
-Hii hutokana na damu kufika kidogo kwenye ubongo hasa pale unapokuwa na tatizo la kiafya.

ii) Mapigo ya moyo kuongezeka.
-Hii ni hasa pale unapokuwa umeketi na kuinuka ghafla kiwango cha damu yako kinakuwa kimebaki sehem ya chini Miguuni na endapo hakutakuwa na hatua yoyote kuchukuliwa na mwili wako husababisha presha yako kushuka na ikiwezekana kudondoka ghafla na hata kuzimia pia.

iii) kushindwa kuzingatia vzuri jambo
-kutokuwa makini eitha na taarifa muhimu upewayo au jambo muhimu la kulifanyia kazi.

iv) Kujihisi kuchoka choka sana na kutapika.

v)Kuvuta pumzi kwa taabu.

AINA ZA PRESHA YA KUSHUKA.

I)ORTHOSTATIC HYPOTENSION.
-Hutokana na kubadili mazingira uliyonayo kwa ghafla mfano.kusimama ghafla kutoka ulipokaa au ulipo lala na huwa haichukui mda mrefu ni sekunde kadhaa mpaka dakika moja.

II)NEURALLY MEDIATED HYPOTENSION(NMH).
*Huwapata zaidi vijana na watoto kutokana na÷
             -Utumiaji wa pombe.
             -Utumiaji mkubwa wa dawa                         za presha ya juu(ya kupanda).
             -Utumiaji wa dawa za nusu kaputi wakati wa kufanyiwa Oparesheni.

III) SEVERE HYPOTENSION.
*Hutokana hasa hasa na kupoteza fahamu.

HALI INAYOSABABISHA PRESHA HII

i) Kuwa na mimba.
ii) Matatizo ya hormoni mwilini(Hormone imbalance).
iii) Maradhi ya Kisukari.
iv) Utumiaji mkubwa wa dawa za hospitali zikiwamo za presha ya kupanda.
v) Maradhi ya Moyo.

0 on: "PRESHA YA KUPANDA NA YA KUSHUKA"