BUNGENI:MBUNGE WA CCM AWAFANANISHA WAPINZANI NA MBWA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Job Ndugai amelazimika kumpokonya Najma Giga uongozi wa kikao cha Bunge baada ya mzozo uliosababbishwa na Mbunge wa CCM aliyewafananisha wabunge wa upinzani na Mbwa.
Mbunge huyo wa Jang’ombe amesema kuwa ukiona majuha wanapongezana wakaona wamefanya la maana, kuna Mbwa kama watatolewa bungeni itakuwa vizuri sana.
“Nasikia milio ya Mbwa humu Bungeni, ukiwatoa itakuwa vizuri sana kwakuwa wanatupigia kelele humu ndani.”amesema Omar
Hata hivyo, Kauli hiyo ilipelekea wabunge wawili kutoka Chadema, Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo na Mchungaji Peter Msigwa wa jimbo la Iringa Mjini kusimama wakitaka utaratibu ufuatwe kwa mchangiaji kuomba radhi.
0 on: "BUNGENI:MBUNGE WA CCM AWAFANANISHA WAPINZANI NA MBWA"