Game Reviews

SOMA BIBLIA UPATE MAARIFA

 


     


MKUMBUKE MUNGU Hata sekunde moja moja kila siku. 
Qn.JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?
Wakatoliki wengi huyumbishwa kwa kuambiwa huamini mambo ambayo hayako au ni kinyume na Biblia. Aya zifuatazo zitakusaidia wewe mkatoliki kuelewa au kujua mistari ya Biblia inayofafanua imani katoliki.
1) KUOMBEA MAREHEMU:
2 Mak. 12:38-46
Hek. 3:1
Tob 4:17

TOHARANI (PURGATORY au UTAKASONI).
1. Kitabu cha "Churches of Today" ukurasa 23 panaeleza kwamba watu walianza kufundisha
habari ya toharani katika karne ya sita. Lakini, mawazo hayo hayakufanywa kuwa ni mafundisho
rasmi ya kanisa mpaka B.K. 1439 kwenye mkutano wa Florence (Council of Florence).
2. Wakatoliki wanakiri wenyewe kuwa hakuna mstari hata mmoja katika Biblia unaofundisha
kwamba kuna mahali panapoitwa toharani.
3. Wakatoliki wanafundisha kwamba, baada ya kufa, watu huingia katika sehemu mojawapo kati ya
sehemu tatu za ulimwengu wa roho.
i. Mbinguni - akaako Mungu;
ii. Toharani (Purgatory) - wakaako watu watendao dhambi ndogo;
iii. Jehenamu - wakaako watu wenye dhambi nyingi.
4. Mwanzoni, walidai kuwa watu wanaoingia toharani watakaa huko mpaka watakaposafishiwa au
kutakaswa dhambi zao kwa njia ya mateso makali.
5. Baadaye, walianza kufundisha kuwa watu wanaokufa dhambini wanaweza kutoka mapema
matesoni mwao kwa njia mbalimbali. Kwa mfano:
􀂃 Ndugu yake akitoa fedha kwa padre ili amfanyie misa ya wafu na kumwombea, basi,
atapungukiwa muda wa kukaa toharani.
- Wanasoma: (2 Makabayo 12:43-46) wakijaribu kujitetea imani hiyo ya kuwaombea wafu.
6. Waumini wanafundishwa waseme: "moyo wa Mariamu niokoe", na kila asemapo hivyo, mfu
atapunguziwa siku mia tatu za kukaa toharani. (Hawana hata mstari mmoja wa Biblia wa kusorna
ili wajitetea mafundisho hayo.)
7. Mtu akienda kanisani kila Jumamosi, ama Mungu atampunguzia miaka 87 ya kukaa kule
toharani, ama Mungu atampunguzia dhambi. (Hapo napo hawana hata mstari mmoja wa Biblia
wa kuyathibitishia hayo.)
8. Kwa maelezo mengine kuhusu chanzo cha mafundisho ya toharani, soma tena uk. 19.

􀂙 MAFUNDISHO YA BIBLIA.
1. Biblia haiseimi lo tote kuhusu mahali panapoitwa toharani. (au purgatory).
2. Wakatoliki wanadai kuwa kitabu cha 2 Makabayo kimetoka kwa Mungu kama vile vitabu vingine
vya Biblia. Walakini, ni kitabu kisichokubaliwa na mamilioni ya watu.
􀂃 Hata Wayahudi wenyewe hawasemi kuwa kimetoka kwa Mungu.
􀂃 Wala hakuna mahali popote katika Agano Jipya ambapo Yesu au mitume waliwahi kudondoa
neno lo lote kutokana na kitabu hicho Pamoja na hayo, hata kama tungalikubali kuwa
kimetoka kwa Mungu, walakini ni kitabu kilichoandikwa katika Kipindi cha Agano la Kale, wala
si Agano Jipya.                      
􀂃 Wakristo tuko chini ya Agano Jipya, na siyo Agano la Kale. Kwa hiyo, hakiwezi kutuongoza
sisi leo.
􀂃 Jambo la mwisho, kitabu hicho kinasema kuwa Yuda Makabayo alipeleka fedha Yerusalemu
kusudi makuhani watoe sadaka za dhambi hekaluni. Hakisemi kuwa tutoe sisi fedha
kanisani kusudi mapadre watoe sadaka za dhambi.
􀂃 Kama tulivyokwisha kujifunza Mapadre sio makuhani. Tena, hawawezi kutoa sadaka kwa ajili
ya dhambi.
3. Hatupati nafasi ya kutubu wala kusamehewa baada ya kufa (Ebr. 9:27; 2:3).
􀂃 Katika (Lk. 16:19-26), Yesu alionyesha kwamba, baada ya kufa, hakuna msaada tena kwa
waliokufa.
4. Kutoa fedha kanisani hakuwezi kuondoa dhambi. (1 Pet. 1:18; Mdo. 8:20).
􀂃 Katika (Mt. 10:8) Yesu alisema: "mmepata bure, toeni bure". Kwa hiyo, ikiwa watu
wangeweza kusamehewa kwa kuombewa na mapadre, basi mapadre wasingepaswa kudai -
- fedha, bali kwa mioyo ya upendo wangejitoa kila siku kuwaombea wafu bure.
5. Hatuwezi kusamehewa dhambi zetu kwa ajili ya matendo mema ya watu wengine; kwani Mungu
amesema: "haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake wenye uovu utakuwa juu
yake" (Eze. 18:20).
􀂃 Kila mtu atahukumiwa kufuatana na matendo yake aliyoyatenda alipokuwa hai (2 Kor. 5:10)
􀂃 Kabla mtu hajafa, anaweza kusamehewa dhambi zake zote kwa njia ya kutubu na kumtii
Mungu (1Yoh. 1:9-10). Walakini, baada ya kufa, Hatupati nafasi tena ya kuokoka.

                                 SOMA   BIBLIA UPATE  MAARIFA

0 on: "SOMA BIBLIA UPATE MAARIFA"